Description
Stadi za Kiswahili ni mfululizo wa vitabu vya kiada vya Kiswahili vilivyoandaliwa kwa kufuata Mtaala wa Umilisi. Kitabu hiki kina sifa kuu zifuatazo:
● Kimeandikwa kwa Kiswahili cha kiwango cha mwanafunzi wa Gredi ya 5.
● Maswali dadisi yametumiwa kutanguliza dhana zilizomo.
● Kimejumuisha shughuli za mwanfunzi binafsi, shughuli za wanafunzi wawili/wawili na za makundi ya wanafunzi.
● Kimeshughulikia masuala makuu yote kwa mujibu wa muhtasari wa Kiswahili cha Gredi ya 5.
● Kimejumuisha mada kuu na mada ndogo zote.
● Yaliyomo yanapangwa kulingana na muundo wa Kiswahili cha Gredi ya 5.
● Yaliyomo yamewasilishwa kwa ubunifu wa kuvutia na kiwango cha juu.
● Kimeshughulikia matokeo makuu yanayotarajiwa katika Gredi ya 5.
● Kimejumuisha umilisi wa kimsingi kwa mujibu wa Mtaala wa Umilisi.
● Kimeshughulikia masuala mtambuko yote.
● Yaliyomo yanakuza maadili yanayopendekezwa katika Mtaala wa Umilisi.
● Shughuli za ujifunzaji zinakuza stadi za kusikiliza na kuzungumza, kusoma na kuandika.
● Michoro na picha za rangi zinachangia yaliyomo kueleweka kwa urahisi.
● Maandishi makubwa na ya rangi mbalimbalim gasonseka kwa urahisi.
Haya na mengine mengi yamegandhamiria kumwezesha mwanafunzi wa Gredi ya 5 kuwasiliana kwa Kiswahili sanifu katika mazingira mbalimbali.